Yona, Gandu, Vuasu Cooperative Union, Same, Tanzania

HISTORIA FUPI YA YONA ELIFADHI YA MAFUNZO YA GALS SHORT STORY OF YONA ELIFADHI ON GALS TRAINING

UTANGULIZI INTRODUCTION

Kwanza kabisa ninapenda kuwashukuru wakufunzi kwa kutufundisha mpango mzuri wa maisha kwani katika mawazo yangu mwenyewe nilifikiria kuwa ili nipate kufanikiwa ni lazima nitafute mfadhili atake nipatia msaada ili niweze kuwa katika hali nzuri kimaisha kumbe sivyo.Kinachotakiwa ni kupata Elimu ili iweze kunisaidia kuboresha maisha yangu na familia kwa ujumla.  First and foremost I would like to thank our trainers for teaching us good life planning skills, I usually thought that, in order for me to succeed in life I must find a sponsor/donor to help me have a good life standard, which I know now it is not the case. All I need is the education that will help me improve my life and my family’s as a whole

NILIVYOANZA HOW I STARTED

Baada tu yakupata mafunzo haya niliangalia ndoto yangu kwanza kwamba ninataka kuwa na maisha ya kiwango gani nikaona kwamba ninahitaji kuwa na maisha mazuri ya kiwango cha juu sio katika hali duni. Baada ya kulifikiria hilo nikaangalia mahali nilipo sasa nikaona kwamba sio pazuri na wala sipapendi kwani sijawa na nyumba nzuri,sijawa na Usafiri wangu mwenyewe, watoto wangu bado hawajasoma na kupata Elimu ya juu hivyo nikaona kuwa ni vyema niwe na mpango mzuri wa maisha. Baada yakugundua yote hayo nikaanza kufuatilia Elimu niliyo ipata nikauliza ujenzi wa nyumba kubwa ambayo mpaka sasa niko kwenye hatua ya kupiga ripu  pia ninaendelea kuboresha mashamba kama vyanzo vya mapato yangu.Na watoto wanaendelea vizuri shuleni kwani wakwanza tayari yuko Sekondari. Pia vile vile ninao mpango mwingine mzuri wa kuanzisha ufugaji wa kuku mpaka sasa nimeshaweka mikakati ya ujenzi  wa banda la kufugia kuku hao na ninao ufugaji mwingine wa mbuzi ambao kwasasa ninao mbuzi watano. Hivyo yote hayo ni matunda ya mafunzo ya GALS mimi binafsi ninayashukuru sana  kwani yananisaidia maishani.

After receiving the training, I first examine my dream and realized that I wanted a high quality of life and not otherwise.  After that I looked at my current life and discovered it is not the standard I desired and I do not like it, as I do not have a good house, my own car and my children have no education. Thus I saw the essence of having a good life plan. Started applying the training received, i enquired what it takes to have a good house, implemented the information and up to now the house am bulding is on final stage. Furthermore I improved the farms as they are my source of income, futhermore my children are doing well in school whereby the firstborn has joined secondary school. Adding to keeping five goats, I also planned to start keeping chicken of which as to now the chicken hut is under construction. All of these are the fruits of GALS training, whereby am grateful as the training has been a mojor help in my life.

NILIOWAPATIA ELIMU NA MIMI THOSE I TRAINED

Baada tu ya kupata elimu hii sikuikalia bali niliendelea kufundisha watu wengine ili kila mmoja apate kusonga mbele kimaendeleo kwa maana hiyo nilifikia watu 40 wa kwanza akiwa ni mke wangu katika hawa 40 waliopokea vizuri ni watu kumi (10) ambao wamechora vizuri kwenye daftari zao na wengine wameshafanikiwa tayri vijana wawili (2) wameshaenda vyuo vya ualimu na mwingine mmoja (1)  chuo cha polisi wengine ni wakulima na wanaendelea kufuatilia malengo yao, hawa wengine waliobakia ambao hawakupokea vizuri ni wale ambao walidhani watapata fedha za ufadhili ili kufanya shughuli zao wakasahau kwamba elimu ndio kitu cha muhimu kwanza ila iko siku wataelewa tu kwa kutokana na mafanikio tunayo yapata sisi.

After receiving this education, I had to share the training with other people so as to help them move forward in life and get development, thus I reached 40 people one of them being my wife. Amoung the 40 I trained, 10 received it very well and have drawn their plan so well in their books. Through the training others have been very successful for example, 2 youths have joined teaching college and 1 has joined Police College. The other 7 people are farmers and have kept track of their plans. Those who did not receive the training well are those with the mentality that, for one to succeeed in life you must have a donor to support, they forget that education is the key. I believe one day they will realize through us who have benefited.

MAONI Opinion

Kazi hii ni nzuri kwani tumeipenda ndiyo maana tumeamua kujitolea tena tunaifanya katika mazingira magumu ya kupanda milima kushuka mabonde kama nilivyoona wakati mlipotuachia changamoto hizi ili tuzidi kusonga mbele zaidi na kupata mafanikio makubwa.

Being a trainer to other is a good work that is why we decided to volunteer even though working conditions are very hard. We have to climb hills up and down as you saw when you left us. We keep on doing these so as to move forward and get great succees

Wako mpenda Maendeleo Yours Sincerely

Yona Elifadhi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.