Mustafa Hoseni Msuya, Vuchama, Vuasu Cooperfative Union, Same, Tanzania

Lead_song_-6

MUSTAFA HOSENI MSUYA
VUCHAMA/NGOSI RCS LTD
S.L.P 1 P O Box MWANGA
SIMU: 0763310339

Personal Statement

Mimi ni mkulima wa mazao mbalimbali katika kijiji cha VUCHAMA kata ya MWANIKO wilaya ya MWANGA, mkoa wa KILIMANJARO. Nilizaliwa mwaka 1964 katika kijiji cha Vuchama. Nimeoa nina watoto saba wakiume 4 na wa kike 3 wote wamesoma hadi kidato cha nne mmoja ni mwalimu mdogo yuko darasa la 7.
I was born in Vuchama village back in 1964, located at Mwaniko ward, Mwanga district in Kilimanjaro region where I still resides. I am a farmer, husband and a father of seven children (4 sons and 3 daughters). The last born is in standard seven and the rest have completed secondary education and one is a teacher
Kwa bahati mbaya mke wangu alifariki dunia mwaka 2002. Niliwajibika kuoa mke mwingine ili anisaidie kulea watoto. Hali hii iliniongezea familia hali ambayo hata mimi sikuipenda. Watoto wote wanasoma na wale wa kike wakubwa anajitegemea kwa sasa pia wananisaidia katika masuala mbalimbali. Unfortunately my wife died in 2002, I had to marry another woman to help me raise the children. The number of headcount increased in my household, something I did not like. My older daughters have own houses, they often assist me and my household because other children are still in school.
Mimi binafsi nafanya kazi katika chama cha Ushirika. Nilianza kazi mwaka 1988 mwaka 1998 niliomba kusimama kutokana na Vuruugu la soko la uria. Mwaka 2008/2009 Bodi iliniita tena baada ya wale walioajiriwa kusababisha hasara, hadi leo nafanyakazi hapo.Nimepata mafunzo mengi kama hivi:
From 1988 I worked at Vuchama /Ngosi Primary society, I resigned in 1998 due to problems brought by the free market. The new primary society employees brought a very big loss which made the Board to hire me again in 2008/2009 in which I still work. During my course of employment I have received different trainings as follows
 Uhasibu chuo cha ushirika – Moshi Accountancy at Moshi Cooperative college
 Huduma ya kwanza ya mifugo chuo cha mifugo – Tengeru Arusha Livestock first aid at Tengeru livestock college-Tengeru Arusha
 Elimu ya kupambana na Ukimwi. Shirika la KIWAMWAKU kwa mafunzo hayo nilianzisha kikundi cha kina mama kupambana na ukimwi.kwasasa niko GALS tangu niingie GALS nimegundua kuwa sikufanikiwa hapo mwanzo kwani sikujua nini maana ya fursa, changamoto nk.HIV/AIDS training through KIWAMWAKU NGO, through this training I established a women group to fight AIDS. Since I received GALS training I have realized that I was not succeeding enough because I did not know the opportunities and challenges that I face
a) Njozi mbalimbali Different dreams and vision
b) Barabara ya malengo kufikia njozi The road to take to reach the dreams
c) Mti wa usawa wa jinsia Gender equality tree
d) Uwezeshaji jamii Community mobilization
e) Mti wa Biashara n.k Business tree e.t.c
Mafunzo niliyopata ya mwanzo yalinipa uelewa mkubwa.Kupanga malengo kwa kuyafikia.Katika mafunzo haya mti wa usawa wa jinsia umeleta msaada mkubwa katika jamii namna ya kufanya kazi kwa pamoja. Nimeanza mafunzo kwa jamii na baadhi yao wamefikia uelewa. The training I received gave a great understanding on setting vision and ways to reach them, furthermore gender equality training have helped the community on how to work together as a team. I have started training others and they understand very well.
Mimi kwa kutumia dhana za GALS nimegundua kwa nini nilikuwa nashindwa kufikia malengo. Through GALS I have discovered why I could not reaching my goals
Changamoto katika kufundisha jamii ni kupewa maji ya kunywa. One of the challenges I face when training other community members is, there is no any allowance provided.
Watu wa eneo letu wanalima zao la kahawa ambalo limeshuka sana na sasa wameanzisha zao la vanilla wengi wao ni wale wanaoshiriki mafunzo ya GALS. Majority of GALS trainees have started vanilla production because profit from coffee has dropped. Most of community members are coffee farmers.
Mafunzo mengine niliyopata ni Uongozi ambayo yamefanya nielewe: – Kanuni za Biashara na Masoko yenye faida. Kabla ya masomo sikuelewa kutafuta masoko,mti wa Biashara,uzalishaji na hesabu zake. Hivi sasa naelewa fursa na changamoto zote. The training that I have received includes leadership, business rules, profitable markets, business tree, production and accounting. I did not know anything about this, now I understand opportunities and challenges in front on me
Chama cha Vuchama kina wanachama 520 wanaoendelea na chama kwa kuuza sasa ni 3. Kwa jinsi mafunzo ya GALS yalivyo baada ya Uongozi kuyapata huenda kwa malengo ya kurudhisha idadi ya mwanzo.Tunajitahidi kuelimisha hadi tutakapofikia lengo. After receiving GALS training, the Vuchama Primary Society leadership set a vision to add more members to exceed 520 present members
Baada ya maelezo yote hayo wakufunzi wetu wameamua kunipeleka Uganda sehemu iitwayo BUKONZO JOINT UGANDA kuona na kujifunza jinsi walivyofikia mafanikio ili turudipo tuendelee kutoa mafunzo tuliyoona na siyo tuliyosikia, pengine itakuwa changamoto kwa wengine. Our trainers took me to Bukonzo joint in Uganda for a field visit to learn how they have succeeded so as to motivate our farmers based on what we saw and learnt
Kwa sasa nipo katika maandalizi ya kwenda Uganda na baada ya hapo nipo tayari kutoa elimu popote ndani na nje ya kijiji,kata,wilaya , mkoa na Taifa na hata nje ya nchi pia nipo tayari kwenda kujifunza popote.Tunaomba uwezeshwaji mara kwa mara. As for now I am in the final preparations to visit Uganda and learn more. After this visit I will be capable to train farmers in other villages, wards, districts, regions and other countries as well. We ask for more frequent trainings in any place.
Asanteni Mwisho The end. Thank you Wenu Yours Mustafa H. Msuya

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.