Iddi Mchome, Chome, Vuasus Cooperative Union, Same Tanzania

P.O.BOX 333, SAME

KILIMANJARO

Simu: 0786 578577/0788 066683

 HISTORIA YA MAISHA YANGU STORY OF MY LIFE

Mimi naitwa Iddy Mchome,Nimezaliwa mwaka 1975 nimesoma darasa la saba 1999, Sekondari  mwaka 2004, kazi kwa sasa mi ni mjasiriamali.

Mafunzo nilipata katika shirika la Swis contact juu ya vicoba na tukaelimisha watu jinsi ya kuungana pamoja na kuunda mfumo wa kuweka na kukopeshana.

I am Iddy Mchome, born in 1975. Finished primary education in 1999 and secondary education in 2004, am entrepreneur.I received training on village cooperative bank (VICOBA) through SWIS CONTACT, from then I started training people on how to build the system of saving and loans.

MALENGO: PLANS

Malengo makubwa yalikuwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kusaidiana. Kwasasa tumefikia kuunda vikundi vinne(4) lengo lingine tuliona tuwashirikishe sana kina mama kwani kina mama wengi wa vijijini wana kipato duni sana ukilinganisha na kina mama wa mjini.

Baadhi ya wakina mama wamefanikiwa kubadilisha maisha yao kwa kusomesha watoto kuinua uchumi wao na biashara na pia kubadilisha mfumo mzima wa maisha yao kwa ujumla na kwa sasa tuna tarajia kuunda vikundi (10) hadi mwaka 2016.

The main plan was to help small scale farmers help each other. As for now we have managed to build four groups. Another plan was to involve women since many village women have low income compared to women from urban areas.

Some of the women have benefited from this by advancing their life, sending children to school, starting small business and develop economically. We have planned to establish new 10 groups by 2016

MAFUNZO YA GALS GALS TRAINING

Nilifanikiwa kupata mafunzo ya GALS kuanzia mwaka 2013 baada ya kupata mafunzo hayo kwanza nilifahamu nini ndoto yangu ni njia ipi ambayo itaniwezesha kukamilisha malengo yangu baada ya kupata elimu, kwanza maisha yangu yalibadilika kutoka nyumba ya vyumba viwili hadi kuwa nyumba ya vyumba 4 na vyoo ndani , baada ya hapo nilifanikiwa kutembelea baadhi ya vikundi mbalimbali kutoa elimu na baadhi ya vikundi vimetambua umuhimu wa mafunzo ya GALS.

I was lucky to receive GALS training in 2013. After this training my dreams and ways to attain them were revealed. Through applying the training my life have changed in a positive way, for instance I moved from a 2 rooms house to a 4 bedrooms self contained house. I visited some VICOBA groups and trained them on GALS as well

NDOTO DREAM/Vision

Ndoto yangu mimi nikutoa elimu kwa kila kaya juu ya ushirikishwaji wa kina mama kupata hati miliki ya nyumba mali pamoja na mambo mengine kwani kina mama wengi wa kiafrica mume anapotangulia familia iliyobakia inanyanyaswa sana. My dream is to educate each household on the importance of women to own house tittle deeds and shared properties, because most African women undergo a lot of discrimination when their husbands die.

MATARAJIO EXPECTATIONS

Matarajio yangu kwa kushirikiana na muwezeshaji wa GALS tutaona umuhimu wa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kumshirikisha mama juu ya hati miliki, baada ya hapo mimi nina washukuru sana GALS na nitakuwa tayari kushirikiana nao katika mafunzo mbali mbali pale nitakapohitajika kwani jamii ya watu wengi bado wanahitaji kuelimishwa. By cooperating with As GALS trainer, I expect to train community on the impontace of involving women on owning house title deeds. Moreover I am grateful to GALS crew, and I wil be available for other training whenever needed because community members still neeed to be educated.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.