Veronica Mchome, Gandu, Vuasu Cooperative Union, Same, Tanzania  

Personal Statement

Chama cha Msingi Gandu Gandu Primary Society, Hedaru, Same, Kilimanjaro Mimi ni Champion VERONICA MCHOME kata ya Hedaru Wilaya ya Same Mkoa Kilimanjro.Nchi yangu Tanzania.

Mimi ni champion wa Chama cha Msingi GANDU VUASU. I am Veronica Mchome a champion at Gandu Primary society at Vuasu which is located at Hedaru ward, Same district in Kilimanjaro region Mimi niliingia mafunzo ya GALS na kuna mambo ambayo nimefanya baada ya kufundishwa. Nilipoanza mafunzo haya nimetimiza mwaka mmoja katika mafunzo haya GALS.

It has been one year since I received GALS training, and I have started applying some of the training already. Ndani ya mafunzo haya nilikutana na fursa na changamoto.Na katika mafunzo haya nimeyapenda kwasababu yamenifundisha mgao wa bajeti katika familia yangu. I like these trainings because have taught me to budget resources in my family. Pia mafunzo haya ni mazuri kwani ni ya mgao katika malengo ya familia zetu na mambo ambayo nimefanya niliona nipange kazi zangu katika miezi mine (4), nilianza na kulima Maharagwe gunia 1 nikapata shs. 50,000/=.Nikaamua nianzishe Biashara ya nguo, ndani ya miezi minne ya pili niliamua nicheze kikoba.

The trainings are good because they have taught us to have vision in our families. After the training I devided my vision into four months period. During the first four months I harvested one sack of beans from my farm and I sold it at Tsh. 50,000. Following that I started a garments selling business. During the second four months I joined VICOBA Katika kikoba nilicheza kistatila siku ya Jumatano nilikuwa ninatoa shs. 5,000/= kila Jumatano. Nilifurahi sana kwasababu niliweza kupangilia mambo yangu mimi mwenyewe.Katika miezi minne ya pili niliulizwa na wenzangu na nikawafundisha. Every Wednesday I was contributing Tsh. 5000 to VICOBA, I was able to plan well my life.

During the second four months my fellows noticed a change in me so I decided to train them as well. Nilipoanza kuwafundisha niliwafundisha majirani, marafiki na watoto waliopenda kusikiliza mafunzo haya ya GALS. Walifurahia mafunzo haya kwasababu walikuwa hawakujua kupangilia mambo yao vizuri lakini wakajua. I started training my neighbours, friends and some children who were interested in listening GALS training. They were all very happy because they learnt to plan, something they never knew. Na katika miezi minne ya mwisho nilipanga katika miaka 3 nitapata TShs.250, 000/= na hapa nilipo katika mwaka wa kwanza nikapata TShs.135, 000/= nilifurahi kwasababu mipango yangu itafikia malengo bila shida. Pia Tshs 135,000/= ni pamoja na kuvuna kikoba. During the last four months I set another plan that, for three years I will save Tsh. 250,000. Am in the first year of my plan and I have already saved Tsh. 135,000 from all sources including VICOBA Mimi nimeona kwamba kupitia mafunzo haya nimeyaona ni mazuri kwani nimepata mabadiliko kwa muda muafaka na pia wale niliyowafundisha walipata mabadiliko kwa muda muafaka kwa ujumla.

Through this training I have observed positive changes both to me and the ones I have trained Kwahiyo tunatarajia kubadilika zaidi kupitia mfumo huu wa mafunzo haya kwasababu yametuwezesha kufahamu umuhimu wa usawa wa jinsia. So we expect to see more positive changes through this training because we now know the importance of gender equality.

Elinazi Eliapenda (Mpole), Bwambo, Vuasu Cooperative Union, Same, Tanzania

 

MUHTASARI WANGU KABLA NA BAADA YA KUPATA ELIMU YA GALS MY STORY BEFORE AND AFTER GALS TRAINING

Mimi Elinazi  Eliapende (Mpole) nimekuwa mkulima mzuri sana wa zao la kahawa tangu mwaka 1981 baada ya kumaliza elimu ya msingi. I Elinazi Eliapende (Mpole) have been a very good coffee farmer since 1981 upon completion of my primary education

Idadi ya miti yangu ya kahawa ni 700 wastani wa kilo ninazopata tangu 1981-2014 ni 1700kgs. Nimeendelea kuwa mkulima hadi mwaka 2012 nilipochaguliwa kuwa Mkulima Kiungo. Mafunzo niliyopata kwa kampuni ya TUTUNZE KAHAWA LTD. Ambapo baada ya kumaliza mafunzo na kuhitimu nilipatiwa cheti toka TaCRI, nilifaidika na mafunzo hayo kwa kuyatumia kwenye shamba langu pamoja na kuwafundisha wakulima wengine katika kikundi change ambao pia waliyatumia mashambani na kufaidika,kabla ya mafunzo hayo nilikuwa nikilima bila malengo bila utaalamu kwa hiyo mavuno yalikuwa kidogo bali sasa ninavuna mavuno mengi na bora. Jumla ya wakulima niliowafundisha na kubadilika ni 27.

I have 700 coffee trees, since 1981-2014 I harvest an average of 1700kg of coffee. I was selected to be a promoter farmer in 2012 through trainings offered by TUTUNZE KAHAWA LTD. After completing the training I was awarded a certificate by TaCRI. Before the training I did not follow good agricultural practices thus harvest were few of low quality. After applying what was trained harvests have improved a lot in terms of quality and quantity. I also trained other farmers both individuals and groups and amoung them 27 have seen a positive change.

ELIMU YA GALS GALS TRAINING

Mnamo mwaka 2012 ndipo nilipopata Elimu (Mafunzo) ya GALS .Mafunzo haya yamenisaidia sana kwani yamenielimisha kuweka malengo kuyafanyia kazi kwa michoro. Elimu hii niliipata kwa mara ya kwanza toka kwa Ndugu Lickson Samwel ambaye alinitia moyo, kunifundisha kuweka malengo  hadi kuwa na mafanikio makubwa ndipo nilipoanza ufugaji wa kuku 60,ng’ombe 2 na sasa kondoo 2 On 2012 I received GALS training from Mr. Lickson Samwel who encouraged me to have vision and draw them in a paper. Through this I managed to start livestock keeping and now I have 2 cows, 2 sheeps and 60 chickens.

AINA YA MAFUNZO NILIYOPATA THE TRAINING I RECEIVED

 1. Ndoto yangu My dream
 2. Michoro kuonyesha mti wa usawa wa jinsia Gender equality tree drawings
 3. Michoro kuonyesha uwezeshaji jamii(kuwafikia wengine) Community mobilization drawings (how to reach others)
 4. Michoro kuonyesha – Mti wa malengo Vision tree drawings
 5. Michoro kuonyesha – Mti wa mafanikio Succees tree drawings
 6. Mchoro kuonyesha – Mti wa Biashara Business tree drawings
 7. Mchoro konyesha – ramani ya masoko Markets map drawings

 

MAFUNZO MENGINE NI OTHER TRAINING

 1. Kiongozi Bora – Uongozi Leadership
 2. Mti wa uzalishaji Production tree

FAIDA NILIYOPATA ADVANTAGES

 1. Nimeonyesha ndoto na kuweka mipango ya kuitimiza I have examine my dreams and set ways to reach them
 2. Nilikuwa natawala familia lakini sasa ninaongoza kwa msaada wa usawa wa jinsia I was bossing my family nowadays I lead it by following gender equality
 3. Nilikuwa najifunza mwenyewe bali sasa nawafundisha wengine I train other community memebers
 4. Sikuwa na malengi ya kazi bali sasa naweka malengo na kujitahidi kuyafikia I had no vision, nowadays I set visions and ways to reach them
 5. Kuonyesha mafanikio kwa kuchora kama ufugani nk Through drawings I can illustrate my success
 6. Kugundua mbinu za kupata masoko na kuyafikia. To discover new methods to get markets

MALENGO VISION

Kuendela kujifunza zaidi kuboresha elimu na kuwafikia wengi zaidi ili kuwapatia elimu hii na kuleta mabadiliko katika uzalishaji wa zao la kahawa pamoja na maisha kwa ujumla katika jamii. To keep on learning and train other community members in order to improve coffe production and life as a whole

MABADILIKO CHANGES

Wakulima wote niliowafundisha wamebadilika katika uzalishaji na maisha ya kifamilia na kuwa na ushirikiano.Nilifundisha watu 27 .Wanaume 15 na Wanawake 12. I have trained a total of 27 farmers (15 male and 12 female), they all have improved farm production and family teamwork

MATARAJIO EXPECTATION

Matarajio yangu nikiwezeshwa kupata Usafiri na posho ninakusudia kuwafundisha watu wengi zaidi Kijiji hadi Kijiji – Kata hadi Kata na Wilaya hadi Wilaya na kuanzia elimu hii ndani na nje ya Tanzania.Ili kufikia watu wengi zaidi ya 50,000 na kuleta mabadiliko. I expect to reach and train 50,000 people and more in different villages, wards, districts and even other countries if I will be given transport allowance and per diem.

PAMOJA TUJENGE UCHUMI. TOGETHER WE BUILD THE ECONOMY

Iddi Mchome, Chome, Vuasus Cooperative Union, Same Tanzania

P.O.BOX 333, SAME

KILIMANJARO

Simu: 0786 578577/0788 066683

 HISTORIA YA MAISHA YANGU STORY OF MY LIFE

Mimi naitwa Iddy Mchome,Nimezaliwa mwaka 1975 nimesoma darasa la saba 1999, Sekondari  mwaka 2004, kazi kwa sasa mi ni mjasiriamali.

Mafunzo nilipata katika shirika la Swis contact juu ya vicoba na tukaelimisha watu jinsi ya kuungana pamoja na kuunda mfumo wa kuweka na kukopeshana.

I am Iddy Mchome, born in 1975. Finished primary education in 1999 and secondary education in 2004, am entrepreneur.I received training on village cooperative bank (VICOBA) through SWIS CONTACT, from then I started training people on how to build the system of saving and loans.

MALENGO: PLANS

Malengo makubwa yalikuwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kusaidiana. Kwasasa tumefikia kuunda vikundi vinne(4) lengo lingine tuliona tuwashirikishe sana kina mama kwani kina mama wengi wa vijijini wana kipato duni sana ukilinganisha na kina mama wa mjini.

Baadhi ya wakina mama wamefanikiwa kubadilisha maisha yao kwa kusomesha watoto kuinua uchumi wao na biashara na pia kubadilisha mfumo mzima wa maisha yao kwa ujumla na kwa sasa tuna tarajia kuunda vikundi (10) hadi mwaka 2016.

The main plan was to help small scale farmers help each other. As for now we have managed to build four groups. Another plan was to involve women since many village women have low income compared to women from urban areas.

Some of the women have benefited from this by advancing their life, sending children to school, starting small business and develop economically. We have planned to establish new 10 groups by 2016

MAFUNZO YA GALS GALS TRAINING

Nilifanikiwa kupata mafunzo ya GALS kuanzia mwaka 2013 baada ya kupata mafunzo hayo kwanza nilifahamu nini ndoto yangu ni njia ipi ambayo itaniwezesha kukamilisha malengo yangu baada ya kupata elimu, kwanza maisha yangu yalibadilika kutoka nyumba ya vyumba viwili hadi kuwa nyumba ya vyumba 4 na vyoo ndani , baada ya hapo nilifanikiwa kutembelea baadhi ya vikundi mbalimbali kutoa elimu na baadhi ya vikundi vimetambua umuhimu wa mafunzo ya GALS.

I was lucky to receive GALS training in 2013. After this training my dreams and ways to attain them were revealed. Through applying the training my life have changed in a positive way, for instance I moved from a 2 rooms house to a 4 bedrooms self contained house. I visited some VICOBA groups and trained them on GALS as well

NDOTO DREAM/Vision

Ndoto yangu mimi nikutoa elimu kwa kila kaya juu ya ushirikishwaji wa kina mama kupata hati miliki ya nyumba mali pamoja na mambo mengine kwani kina mama wengi wa kiafrica mume anapotangulia familia iliyobakia inanyanyaswa sana. My dream is to educate each household on the importance of women to own house tittle deeds and shared properties, because most African women undergo a lot of discrimination when their husbands die.

MATARAJIO EXPECTATIONS

Matarajio yangu kwa kushirikiana na muwezeshaji wa GALS tutaona umuhimu wa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kumshirikisha mama juu ya hati miliki, baada ya hapo mimi nina washukuru sana GALS na nitakuwa tayari kushirikiana nao katika mafunzo mbali mbali pale nitakapohitajika kwani jamii ya watu wengi bado wanahitaji kuelimishwa. By cooperating with As GALS trainer, I expect to train community on the impontace of involving women on owning house title deeds. Moreover I am grateful to GALS crew, and I wil be available for other training whenever needed because community members still neeed to be educated.

 


Nicolaus Abraham, Gandu, Vuasu Cooperative Union, Tanzania

Gandu_Abraham-1
Abraham showing how far away he lives from Gandu cooperative centre. Right up on the distant mountain by another road.

Personal Statement

0755672344

Nicolaus Abraham ni mmoja wa wanachama wa GALS ambao mliwafundisha, katika ndoto yake kwa mwaka 2014 ni kujenga nyumba yake ya vyumba vitatu na sebule katika ndoto yake alikuwa na nyumba ya vyumba viwili.Lakini kabla hajapata mafunzo ya GALS hakuwa na mpango wa kujenga nyumba nyingine kwa mwaka 2014.Baada ya kupata mafunzo haya aliamua kubomoa na kujenga nyumba nyingine ya vyumba vitatu na sebule kwa mwaka 2014 baada ya mafunzo. Ili kutimiza ndoto yake.

Nicolaus Abraham is one of the GALS champions. His dream of 2014 is to build a house with three bed rooms and a living room, in reality he has a two rooms house. Before receiving GALS training he had no plans of building a house on 2014. After the training he decided to build his dream house of three bedrooms and a living room on 2014 in order to live his dream.

MALENGO, FURSA NA CHANGAMOTO VISION, OPPORTUNITY AND CHALLENGES

MALENGO:     Ni kutoka Kwenye vyumba viwili hadi kufikia vyumba vitatu na sebule ya kisasa katika barabara ya malengo alikuwa na fursa zifuatazo:

VISION: To move from a two rooms house to a three bedrooms and living room house, towards working on his plan he had the following opportunities:

(a)   Ng’ombe  2 2 cows

(b)   Kuku  20 20 chicken

(c)   Fedha Money 3,500,000                             3,500,000/=

(d)   Kilimo cha maharagwe ekari         3 3 acres of beans farm

(e)   Kilimo cha fiwi ekari                      2 2 acres of lablab farm

(F)   Kilimo cha mahindi ekari   3 3 acres of maize farm

Ilikufikia barabara ya malengo itakayomfikisha Kwenye ndoto yake fursa hizi alizigawanya katika vipindi vitatu Kama ifuatavyo: in order to work on his plan to make him live his dream, these opportunities were devided on three timelines as follows:

MWEZI WA TATU – MWEZI WA SITA MARCH-JUNE

Aliuza ng’ombe moja kwa thamani ya Tshs Laki tano na ishirini elfu (520,000/=).Mwezi wa tatu hadi wa sita akauza tena kuku watano kwa thamani ya Tshs.75,000/=. Mwezi huo huo wa tatu hadi wa sita katumia Fedha ya ziada Tshs. 2,095,000/= (Milioni mbili na tisini na tano elfu).

Between March and June he sold one cow at a price of Five hundred and twenty thousands shillings (TSH. 520,000/=), five chicken at TSH. 75,000/= and spent TSH 2,095,000 from his personal savings.

MWEZI WA SITA – MWEZI WA TISA JUNE-SEPTEMBER

Alitumia fursa zake kama ifuatavyo: He used his opportunities as follows

 • Feza za akiba million 1,000,000 Personal savings TSH. 1,000,000
 • Maharagwe gunia tano 750,000 5 sacks of beans TSH. 750,000
 • Fiji gunia 3 kwa shs 380,000 3 3 sacks of lablab TSH. 380,000
 • Mahindi hakufanikiwa kuvuna He did not harvest any maize

Hivyo kwa mwezi wa sita hadi wa tisa alifanikiwa kupata takribani Tshs 2,130,000/= (Milioni mbili na laki moja na thelathini elfu). Therefore between June and September he was able to collect approximately TSH. 2,130,000

MWEZI WA TISA HADI WA KUMI NA MBILI SEPTEMBER TO DECEMBER

1)         Alitumia akiba ya shs 1,000,000 He used his personal savings TSH.1,000,000

2)         Ng’ombe moja shs       610,000 He sold 1 cow at TSH. 610,000

                                    Jumla  1,610,000 Total 1,610,000

Hivyo Jumla alipata Tshs milioni na laki sita na elfu kumi.

Katika barabara ya malengo alikusudia kujenga nyumba yenye thamani ya milioni kumi na tatu na laki tano. Lakini kwa awamu tatu alifanikiwa kupata milioni sita laki nane na elfu thelathini na tano.Hivyo mgawanyo wake ni kama ifuatavyo: He planned to build a house worth TSH 13,500,000. However for the first phase he managed to collect TSH 6,835,000, thus he devided it as follows:

 • Mwezi wa tatu hadi wa sita boriti                                     1,360,000
 • Mwezi wa sita hadi wa tisa tofali 400                                         800,000
 • Mwezi wa tatu hadi wa sita bati 45                                          675,000
 • Mwezo wa tisa mawe tani 3                                          500,000
 • Mwezi wa tisa hadi wa kumi na mbili ujenzi 1,000,000
 • Misumari                             150,000
 • Fundi kupaua                                           500,000
 • Frem milango na madirisha                                          400,000
 • Shata mlangoni na dirishani                                          502,000

                                                                        Jumla              5,887,000

 • March to june boroti 1,360,000
 • From June to September he bought 400 bricks 800,000
 • From March to June he bought 45 iron sheets 675,000
 • On September he bought 3 tones of stones 500,000
 • September to December he paid for construction 1,000,00
 • Nails                                                                        150,000
 • Payment to roofing technician                      500,000
 • Doors and windows frames 400,000
 • Door and windows shutters 502,000

TOTAL                                     5,887,000

CHANGAMOTO CHALLENGES

Katika barabara ya malengo alipata changamoto ambazo hakuweza kufikia malengo yake nazo ni: the following were the challenged he encountered as he was implementing his plan

 • Ukame Drought
 • Magonjwa Diseases
 • Shule School fees
 • Magonjwa ya Mifugo Livestock diseases

Mpango wake ni kumalizia nyumba yake kwa mwaka 2015 kwa fursa nyingine zilizobaki na kuongeza kilimo kama hali ya hewa itakua nzuri. His plan was to finish building his house by 2015 by utilizing other remaining opportunities and increasing energy in agriculture if drought will not strike.

MTI WA JINSIA  GENDER TREE

KAZI ANAZOFANYA YEYE KAMA BABA NI TASK HE DOES AS A FATHER ARE

 • Ufugaji wa Ng’ombe Livestock keeping
 • Kilimo cha fini tambarare
 • Kukata kuni na kuzipasua na kuuza preparing and seeling firewood
 • Kupika tofali making bricks
 • Uchomaji wa Tofali

KAZI ANAZOFANYA MAMA YEYE MWENYEWE TASKS MOTHER DOES ON HER OWN

 • Kupika cooking
 • Kufua laudry washing
 • Kufagia cleaning the house
 • Kuosha vyombo Dish washing
 • Kuogesha watoto shower the children
 • Kuchota maji fetching water

KAZI WANAZOFANYA KWA PAMOJA TASKS DONE BY BOTH

 • Kubeba kuni Carring the firewood
 • Kilimo cha maharagwe beans cultivation
 • Kilimo cha mahindi maize cultivation
 • Kuwapa kuku chakula feeding the chicken
 • Kupiga nguo pasi laudry ironing

Chambua Coleman, Chome, Vuasu Cooperative, Same Tanzania

Coleman is a trained extension officer. He gets trainings from the government and other NGOs and sometimes TaCRI (Tanzania Coffee Research Institute) and trains voluntarily for the government on extension. He is not paid for this but gets reimbursement of costs. His motivation is to get certificates. He suggests that obtaining Certificates as GALS trainers would help both to show for further GALS expansion to other villages and other cooperatives as well as for jobs.

He was taught GALS by Hawa Arckland, He has only taught 1 person, he thinks he still needs to understand properly. He has been very busy organising agricultural fairs for the government in the village. He suggested that in the next fairs he will organise trainers to talk about GALS. About 500 people turn up for the fair while the fair is going on normally other crop producers like cabbage growers turn up and he suggested that one GALS trainer could cover one crop producers and share while the fair is going on.

Reverend Mchome Julius WiliJohn, Chome, Vuasu Cooperative Union, Same, Tanzania

 

Reverend Julius Wili John was formerly a seventh day Adventist. But he got a calling through the assemblies of God ministry and started a church. His wife is also a preacher. As wife of reverend her role is to support and conduct counselling sessions to women.

Julius was taught GALS by Hawa Arckland. His vision is to be a bishop. On his Vision Journey he decided to do an onion farm – that he has now achieved.

Chome_Reverend_VJ

Chome_Reverend_Onions-3

Chome_Reverend_GBT-3

Before GALS he and his wife attended trainings from Adra Tanzania with Ministry of Health. The trainings were conducted from house to house advising people on many issues including food security, education, HIV/AIDS and Land rights. All women should know responsibilities in house like children need to go to school, women should clean house, should have rights to ownership of property and earn money together. They plan for school fees and other household issues together. On gender balance his wife is happy and she says they share most of the responsibilities. They own assets together including land. They have a temporally land title signed by the village chairman indicating all assets belong to the family. Even if he dies the village office recognises the wife as the heir.

Julius has taught Philemon Wilfred, his wife and other two group members.The wife was interested to learn livelihood tools.

Personal Statement

P.O.BOX 333 SAME

SIMU: Mobile 0786 114 105/0768 506 863

Mimi mch. Julius ni mzaliwa katika kijiji cha Marieni Tar 20/02/1965. Nimefanikiwa kuoa mwaka 1993,nimepata watoto 5 wakike mmoja na wakiume wanne.Mimi kama mchungaji nimefanya kazi ya kumtumikia Mungu kwa muda mrefu. I was born on 20th February 1965 at Marieni village. In 1993 I got married and blessed with 5 children, 4 sons and 1 daughter. For long I have been saving God as a reverend.

Baada ya kupata mafunzo ya GALS niliyopatiwa kutoka kwa mkufunzi Hawa yamenipa fursa ya kuniwezesha kutambua na kufahamu mambo mengi sana likiwemo swala la kiongozi bora. Nimeamini kuwa kiongozi ni kuwa mfano kwa wale unao waongoza kwa nafasi tofauti tofauti, Mfano mimi ni mchungaji ni naye ongoza watu 67 wanaume 23 na wanawake 44.Pia kati yao kuna wamama wajane 5 na watoto yatima 12, mimi kama kiongozi nimefanikiwa kuwafundisha ndoto na malengo kimaisha na pia kuwaonyesha barabara ya mafanikio bila kusahau mti wa usawa wa kijinsia.  GALS trainings have opened my mind to different things one of them being leadership. I believe now that, being a good leader one has to be a good example to the people he is leading. As a reverend I lead 67 people, 23 men and 44 women whereby amoung them there are 5 widows and 12 ophans. I have trained this congregation on the importance of having dreams and vison in life, the road to success and gender equality tree.

Changamoto ninazo kutana nazo mimi kama mchungaji, nakutana na  watu wenye magonjwa sugu na matatizo mbali mbali. As a reverend I face challenges such as I meet people with chronic diseases and other different  problems

Malengo niliyonayo ni kuwa na Usafiri utako niwezesha kupeleka elimu kwa washirika walioko maeneo mbali kama Tae wapo 9 na Vudee 12 kuhusiana na swala la kuwaelimisha juu ya ndoto,malengo na barabara ya mafanikio, bila kusahau mti wa usawa wa kijinsia. If I will be assisted to get my own transport, I plan to reach other people who are far from where I am, for example in Tae there are 9 people and in Vudee there are 12 people who are ready to be trained on dreams, visions, success road and gender equality tree.

Wako Mchungaji Julias Yours Rev. Julias

 

Lilian and Evalina Mtaita, Chome, Vuasu Cooperative, Same Tanzania

Lilian Mtaita was among the first champions at the Vuasu Catalyst Training in October 2013. After the training she went back to school because her vision was to study nursing and become a good nurse. But she taught GALS to her mother, Evalina Julius.
Chome_Lilian-1

Evelina has learnt good farming practices and livestock through her Vision journey. Lilian and her mother are now keeping exotic cows, which her mother planned through her Vision Journey.

Chome_Lilian-2
Lilian explained to her mother the Gender Balance Tree. They saw that if they work together on one thing they can increase income. She used to use an axe to get firewood for household now her husband does. He also helps with cooking eg while she comes to meetings. The family is in the process of registering land at village office.

Together they did the Leadership empowerment map. Evelina learnt more tools and trained 30 other people trained in her VICOBA savings and credit group. They have introduced her to other crops etc.